JOHN Bocco, mzawa na mfungaji bora wa muda wote kwa wazawa kibindoni amefikisha jumla ya mabao 130 ndani ya Ligi Kuu Bara akitumika ndani ya timu mbili Bongo.
Ametumia miaka 10 kuparanganyika ndani ya Azam FC ambapo akiwa huko alifanikiwa kuwa mfungaji msumbufu na asiyechoka jambo lililowavutia Simba na kumvuta kikosi cha kwanza.
Akiwa na Azam FC alitupia jumla ya mabao 87 kibindoni yaliyompandisha chati nahodha huyo wa Simba.
Mabao 43 ameyatupia akiwa ndani ya Simba ambayo ameitumikia kwa misimu minne ya soka lake la ushindani.
Mabeki wengi Bongo pamoja na washambuliaji wamekuwa wakimzungumzia Bocco kuwa mchezaji wa mfano ndani ya uwanja pamoja na nje ya uwanja kutokana na nidhamu yake.
Dickson Job, beki chipukizi anayecheza ndani ya Mtibwa Sugar ameweka wazi kuwa katika maisha yake ya soka amekuwa akipiga hesabu ndefu namna ya kukabiliana na mzawa huyo.
“Nimekutana na washambuliaji wengi wenye uwezo ila Bocco ni habari nyingine, hajua kuhusu kukata tamaa wewe mpige mabuti unavyoweza anakutazama kisha anaendelea na majukumu yake unaweza kudhani amekuacha, anakuja tena”