MMOJA wa wachezaji maarufu nchini Argentina ambao ilijivunia kipaji cha kipekee, madoido ya ajabu akiwa uwanjani, maono na kasi yalivyovutia mashabiki wengi, alikuwa Diego Armando Maradona.
Lakini pia alisababisha hasira na goli lake alilolipa jina ‘Hand of God’ ambalo lilizua utata pamoja na yeye kutumbukia katika utumiaji wa dawa za kulevya na mapungufu mengine yaliyojitokeza baada ya kustaafu soka.
Mfupi lakini imara – Nyota wa kandanda
Alizaliwa miaka 60 iliyopita huko Buenos Aires eneo la kitongoji duni. Maradona aliepuka umaskini wakati akiwa kijana kwa kuwa nyota wa mpira wa soka ambaye kuna wale wanaomchukulia kuwa bora zaidi akilinganishwa na mchezaji Pele wa Brazil.
Mchezaji huyo wa Argentina, aliyefunga magoli 259 katika mechi 491 alizoshiriki alimshinda mpinzani wake wa Marekani Kusini katika kura ya maoni ya kuamua mchezaji wa karne ya 20 kabla ya Fifa kubadilisha sheria za upigaji kura na wote wawili wakatunukiwa hadhi hiyo.
Maradona alionyesha uwezo wa hali ya juu tangu akiwa mtoto na kuwa chanzo cha timu ya vijana ya Los Cebollitas kuwa kidedea kwa kupata magoli 136 bila kufungwa na timu yoyote na kujitokeza kwake kama mchezaji wa kimataifa akiwa na umri wa miaka 16 na siku 120.
Akiwa mfupi na imara, futi 5 na inchi 5, uchezaji wake haukuwa wa kawaida. Lakini ujuzi wake, wepesi, maono, jinsi alivyodhibiti mpira, alivyopiga chenga na kupitisha mpira kwa wengine kwa sababu ya kukosa kasi na wakati mwingine hata kuwa na matatizo ya uzito wa kupita kiasi.
Huenda alikuwa na kasi ya ajabu akiwa uwanjani karibu na mahasimu wake lakini alikuwa na wakati mgumu kukwepa changamoto
Goli maarufu la ‘Hand of God’ na ‘Goli la Karne’
Maradon alimfunga kipa wa England kwa kufunga na mkono na goli hilo lilikubalika mwaka 1986.
Maradona alifunga magoli 34 kwa kushiriki mechi 91 kama mchezaji wa Argentina.
Yeye ndiyo chanzo cha nchi yake kuibuka na ushindi katika Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico na kupata fursa kuingia fainali miaka minne baadaye.
Katika robo fainali ya mchezo wa awali kulijitokeza utata ambao kumbe baadaye ungekumba maisha yake.
Mechi dhidi ya England ilikuwa na mkwaruzano uliopitiliza kidogo huku vita vya Falklands kati nchi hizo mbili vikiwa vimetoka miaka minne tu nyuma.
Hilo lingesababisha hali uwanjani kuzua wasiwasi zaidi.
Dakika 51 zikiwa zimekatika na hakuna timu iliyoona lango la mwingine, Maradona aliruka na mlinda lango wa timu pinzani, Peter Shilton na kufunga kwa kupiga mpira hadi kwenye neti.
Baadaye alisema goli hilo lilitokana na “Maradona kuupiga mpira kwa kichwa kidogo na mkono wa Mungu”.
Dakika nne baadaye, alifunga kile ambacho kimekuwa kikitambuliwa kama ‘goli bora la karne’ baada ya kuchukua mpira mwenyewe na kuanza mbio kwa kasi ya ajabu ambako kuliacha wachezaji kadhaa wakimfuata nyuma kabla ya kumzunguka Shilton na kufunga bao.
Maradona amefariki akiwa na umri wa miaka 60, siku za mwisho alikuwa alifanyiwa upasuaji wa ubongo akiwa anaedelea vizuri na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kifo kimemkuta akiwa nyumbani, mara baada ya kupata kifungua kinywa juzi, Maradona akamuita mpya wake, Johny Esposito na kutamka maneno mafupi,’ Me siento mal’ akimaanisha kuwa hajisikii vizuri kisha akarejea kitandani kulalala.
Taarifa zinaeleza kuwa gwiji huyo alipata shambulio la moyo. Pumzika kwa amani Maradona.