CHAGUO namba moja la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, mechi 11 zote ameanza kikosi cha kwanza ambazo Simba imecheza kwa msimu huu wa 2020/21.
Amefanya makosa matatu yaliyosababisha timu yake kufungwa mabao matano, kosa la kwanza ilikuwa Kwenye mchezo dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine wakati Simba ikishinda mabao 2-1 katika harakati za kuokoa mpira alianua majaro, ngoma ilikutana na mchezaji wa Ihefu akamtungua Aishi Manula alikuwa ni Omary Mponda.
Kosa la pili ilikuwa wakati Simba ikifungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela, alimpoteza Aishi Manula kwenye harakati za kuokoa hatari mpira wa juu uliokutana na kichwa cha Salum Mbangula.
Kosa la tatu ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga kwa kumchezea faulo Tuisila Kisinda iliyoleta penalti iliyofungwa na Michael Sarpong naye alifunga pia bao lake la kwanza kwenye dabi hiyo.
Kwa sasa Simba ina kibarua cha kuiwakilisha nchi kimataifa ambapo leo inatarajiwa kuanza safari kuelekea Nigeria ambapo kitapitia Ethiopia kabla ya kuunganisha mazima mpaka Abuja Nigeria siku ya Jumatano.
Kazi kubwa kwa Sven itakuwa ni kwenye safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao kwa kuwa inakutana na timu yenye safu kali ya ushambuliaji jambo linalohitaji umakini zaidi.