Home Uncategorized USHINDI MBELE YA WANAIGERIA WAIPA MATUMAINI SIMBA KUTUSUA KIMATAIFA

USHINDI MBELE YA WANAIGERIA WAIPA MATUMAINI SIMBA KUTUSUA KIMATAIFA

[the_ad id="25893"]


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa namna ambavyo wameanza kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya mabingwa baada ya kushinda jana, Novemba 29 bao 1-0 mbele ya Plateau United wana imani watafika hatua ya makundi.

Kikosi hicho kinachonolewa na Sven Vandenbroeck kesho kinatarajiwa kuwasili Bongo baada ya kumaliza dakika 90 za mwanzo wakiwa ugenini nchini Nigeria wana dakika 90 nyingine Uwanja wa Mkapa.


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, ambapo Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele ila ikifungwa itakuwa na kibarua kizito cha kupata ushindi ikiwa, itafungwa bao moja zitaongezwa dakika na mshindi asipopatikana ngoma itakwenda matuta kwa kuwa itakuwa ni 1-1.

  Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa ushindi ambao wameupata na namna mazingira yalivyokuwa magumu yanawapa nafasi ya kupata matokeo mazuri na kupenya hatua ya makundi.


“Tumeanza vizuri na ni matumaini yetu kwamba ni Mungu amejibu maombi yetu hivyo kwa namna ambavyo tumepata ushindi katika mazingira tuliyopitia inamaanisha kwamba tutafika mbali.


“Kikubwa ninawapongeza wachezaji wetu kwa namna ambavyo wamepambana wanapaswa waendelee hivyo ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.

SOMA NA HII  ASTON VILLA MAMBO MAGUMU KWELIKWELI NDANI YA LIGI KUU ENGLAND

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here