Home Uncategorized REKODI ZA SIMBA KWA MKAPA KIMATAIFA NI BALAA, WAARABU WALIKAA

REKODI ZA SIMBA KWA MKAPA KIMATAIFA NI BALAA, WAARABU WALIKAA


 REKODI ya Simba katika michuano ya kimataifa inapocheza katika uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa, imeonekana kuibeba zaidi timu hiyo kuelekea mchezo wake wa marudiano dhidi ya Plateau United, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii Desemba 5.

 

Na inaaminika kuwa kama Wekundu hao waliweza kuwafunga Al Ahly bao 1-0 Dar, basi itakuwa ngumu zaidi kwa Plateau kuchomoka.

 

Simba katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu uliochezwa Novemba 29 nchini Nigeria, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Clatous Chama.

 

Simba katika michezo saba iliyopita ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika nyumbani, haijapoteza mchezo hata mmoja nyumbani na katika michezo hiyo saba, imefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo mitano huku ikitoa sare miwili ya mwisho.


Hata hivyo, timu hiyo imeonekana kuwa na uwiano mzuri wa kufunga mabao ikiwa na wastani wa kufunga mabao mawili katika kila mchezo kutokana na Simba kufunga jumla ya mabao 14, katika michezo hiyo saba huku ikiwa imefungwa mabao matatu.

 

Matokeo ya Simba katika michezo saba ya mwisho nyumbani yalikuwa hivi, Simba 4-0 Mbabane Swallows, Simba 3-1
Nkana, Simba 3-0 JS Soura, Simba 1-0 Al Ahly, Simba 2-1 AS Vita, Simba 0-0 TP Mazembe, Simba 1-1 UD Songo.


Hata hivyo, Simba katika michezo yake miwili ya mwisho haikufanikiwa kuibuka na ushindi wowote baada ya kutoa sare na timu ya TP Mazembe kisha kupata sare nyingine  dhidi ya UD Songo.

SOMA NA HII  SIMBA 6-0 VITAL'0 YA BURUNDI, KIKOSI CHA KWANZA CHATUPIA MAWILI, CHA PILI MANNE