Home Uncategorized SIMBA WATUA KIBABE ZIMBABWE,SERIKALI YAWAPOKEA, MPANDA MPIRA AKOSEKANA

SIMBA WATUA KIBABE ZIMBABWE,SERIKALI YAWAPOKEA, MPANDA MPIRA AKOSEKANA


 WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Simba, leo Desemba 18 wamewasili salama nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa hataua ya kwanza dhidi ya FC Platinum.


Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na kocha msaidizi Seleman Matola kimepata bahati ya kuonana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Profesa Emmanuel Mbennah.


Balozi huyo alipata nafasi ya kupiga picha ya pamoja na viongozi, wachezaji na benchi la ufundi baada ya chakula cha mchana.

Pia amepata nafasi ya kuongea na wachezaji wa timu ya Simba ambao wana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Kikiwa kimeongozana na wachezaji 24 wanaoongozwa na nahodha John Bocco pamoja na Mohamed Hussein, ‘Tshabalala’ atakosekana mpanda mpira Bernard Morrison na Charlse Ilanfya ambao hawapo kwenye mpango wa Sven.

SOMA NA HII  VIGINGI VITATU MATATA KWA YANGA HIVI HAPA