Home Uncategorized YANGA KUMVUTA NYOTA WA KAZI KUMPA SAPOTI YASSIN

YANGA KUMVUTA NYOTA WA KAZI KUMPA SAPOTI YASSIN


 BAADA ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili Desemba 16 tayari uongozi wa Yanga umeingia katika mazungumzo na beki wa kushoto wa Namungo FC, Edward Charles Manyama katika kuiimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.

 

Yanga wanapambana kuhakikisha wanapata saini ya beki huyo aliyewahi kucheza ndani ya kikosi cha timu hiyo katika msimu wa 2014/2015 kabla ya kuachana na timu huyo na kwenda JKT Tanzania na sasa Namungo.

 

Manyama Jumatatu aliifungia timu yake bao la kusawazisha kwa faulo iliyozama moja kwa moja akiwa nje ya 18, wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

 

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Yanga zinadai kuwa Manyama anahitajika na Yanga kwa kuwa ni mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze ambaye anaamini atakuwa msaada ndani ya kikosi hicho kutokana na umbo lake.

 

“Uongozi kwa sasa upo naye kwenye mazungumzo kwa sababu bado ana mkataba na Namungo sasa mwenyewe mchezaji akiwa tayari nadhani watafuata taratibu za kiuongozi kwa ajili ya kumalizana naye na uzuri ameshacheza Yanga miaka ya nyuma hivyo atakuwa anarejea nyumbani.

 

“Unajua sababu kubwa wanamtaka kwa ajili ya kumpa changamoto Yassin Mustafa, huku wakiwa kwenye mipango ya kumtoa kwa mkopo Adeyum Saleh,” alisema mtoa taarifa.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said alipotafutwa kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Tayari yapo baadhi ya majina kwenye mipango yetu ya usajili na hivi sasa tupo kwenye taratibu za mwisho za kukamilisha.

SOMA NA HII  SIMBA YAKIONA CHA MOTO LEO TAIFA, YAAMBULIA POINTI MOJA MBELE YA WAZEE WA KUPAPASA