NYOTA wa Klabu ya Namungo FC, Sixtus Sabilo amesema kuwa ana imani kwamba timu hiyo itatinga hatua ya makundi ndani ya Kombe la Shirikisho kutokana na mwanzo ambao wameanza nao.
Namungo ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal Elobied mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.Inatarajia kurudiana nao kati ya Januari 5-6 nchini Sudani.
Mabao katika mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wawakilishi hao wa Tanzania yalifungwa na Stephen Sey dakika ya 30 na lile la kwanza lilifungwa na Sabilo dakika ya 13.
Nyota huyo mzawa alikuwa mwiba kwa mabeki wa Sudani jambo ambalo liliwafanya wapate tabu kwenye kumzuia ndani ya Uwanja.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sabilo amesema kuwa kuanza kwa ushindi licha ya kwamba ni mdogo ni mwanzo mzuri kwao na wanamini watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wa marudio.
“Tumeanza vizuri imani yangu ni kwamba tutaendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo, mashabiki waendelee kutupa sapoti.
“Matumaini yetu tutatinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, makosa ambayo tumeyafanya nina amini kwamba benchi la ufundi limeona na litayafanyia kazi”.
“Matumaini yetu tutatinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, makosa ambayo tumeyafanya nina amini kwamba benchi la ufundi limeona na litayafanyia kazi”.