Home Uncategorized SIMBA KUREJEA BONGO KUIVUTIA KASI MAJIMAJI

SIMBA KUREJEA BONGO KUIVUTIA KASI MAJIMAJI

 


KIKOSI cha Simba leo kinatarajiwa kurejea nchini Tanzania baada ku kuweka kambi nchi Zimbabwe ambapo kilikuwa huko kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Kinarejea kikiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wake mbele ya FC Platinum kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum.

Kina kazi ya kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Januari 6, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wao unaofuata kwa sasa ambao wataanza nao ni dhidi ya Majimaji FC ya Songea, Uwanja wa Mkapa ambao ni wa Kombe la Shirikisho. 

Itakuwa ni Desemba 27 kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya kusonga hatua ya nne ambayo wapinzani wake wakubwa Yanga wameshapenya baada ya Singida United kushushwa madaraja mawili.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na Seleman Matola ambaye ni mzawa ni mabingwa watetezi wa kombe hili la Shirikisho.

Walitwaa baada ya kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Klabu ya Namungo FC ambayo yenyewe ilishika nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  SIMBA: TUNAFUNGA HESABU JUMLAJUMLA ZA UD SONGO TAIFA