SAIDO Ntibanzokiza ingizo jipya ndani ya Klabu ya Simba akitokea nchini Burundi kwa kusaini dili la miaka miwili amesema kuwa atashirikiana na wachezaji wenzake ili kufanya vizuri zaidi.
Amefunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.Mchezo wake wa kwanza ilikuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji ambapo alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.
Mchezo wake wa pili ilikuwa ni dhidi ya Ihefu FC ambapo alitoa jumla ya pasi mbili za mabao Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Nyota huyo amesema kuwa atashirikiana na wachezaji wenzake kuendelea kufanya vizuri.
“Bado kuna kazi ya kufanya ndani ya Yanga, nina amini kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo nami nitafanya hivyo.
“Kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu nina amini kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” .