CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wana kazi kubwa ya kufanya ndani ya mzunguko wa pili baada ya kukamilisha ule wa kwanza kwa kucheza mechi 17 bila kupoteza mchezo kwa msimu wa 2020/21.
Yanga imeshinda mechi 13 na kulazimisha sare nne ndani ya uwanja na kibindoni imekusanya jumla ya pointi 43 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo.
Inaanza safari ya kuhesabu jumla ya mechi 17 za mzunguko wa pili Desemba 31 ambapo itamenyana na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela,Rukwa.
Kaze raia wa Burundi amesema kuwa kumaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza ni jambo linalohitajika kuendelea pia kwa mzunguko ujao kwa wachezaji wake kupambana zaidi.
“Pongezi kwa wachezaji wangu kwa kupambana ndani ya uwanja na kuweza kupata matokeo ndani ya mzunguko wa kwanza hivyo ni wakati wetu wa kuweza kufanya vizuri kwa wakati ujao.
“Tupo imara na hilo lipo wazi kuanzia mchezaji mmojammoja wote wamekuwa wakijitahidi kufanya kile ambacho tunakihitaji jambo ambalo linatupa matokeo chanya,” .
Ikiwa ipo nafasi ya kwanza wapinzani wake Simba wanawafuatia nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 14 wamekusanya pointi 32.