Simba SC

MAJEMBE YA KAZI SIMBA YATUA

admin August 9, 2021 6:43 am


 NYOTA wa Simba, Clatous Chama amerejea ndani ya ardhi ya Bongo akitokea Zambia ambapo alikuwa kwa ajili ya mapumziko.

Chama ambaye ni kinara wa kutengeneza pasi za mwisho hivi karibuni ilionekana kuwa amezinguana na mtu ambaye anadhaniwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohammed Dewji, ‘Mo’ katika ukurasa wake wa Instagram.

Ilikuwa ni kwenye Instagram Live alipohojiwa kuhusu Haji Manara alimsifia jambo ambalo lilimfanya bosi huyo aombe kuondoka kwenye mkutano huo.

Chama alitoa ufafanuzi kwamba alikuwa kwenye drama ambayo hakuifikiria na wengi wanapenda kuona timu inakuwa kwenye migogoro jambo ambalo halipaswi kupewa nafasi.

Pia Perfect Chikwende naye ambaye ni kiungo amerejea ikiwa ni kwa ajili ya kuweka kambi ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Morocco.

Chikwende alikuwa Zimbabwe ambapo alikwenda kwenye majukumu ya timu ya taifa na ameshamaliza kazi amerejea kuendelea na kazi yake ndani ya Simba ambao ni mabingwa wa ligi.


ALI MAYAI AMVAA MANARA, AMTAKA KUACHA ‘UJANJAUJANJA; NA KUTAFUTA HURUMA KWA MASHABIKI KIUNGO WA UGANDA AUCHO KUMALIZANA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply