Uncategorized

SVEN AWAKA SIMBA, ATAKA KUBEBESHWA ZIGO LA LAWAMA

admin December 28, 2020 9:47 am


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa lawama zote kuhusu uwezo wa wachezaji wake ndani ya uwanja apewe yeye na hataki kuona kwamba kuna watu ambao watawakosoa wachezaji wake.

Kocha huyo jana Desemba 27 alikiongoza kikosi chake cha Simba kushinda mabao 5-0 dhidi ya Majimaji kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya tatu na kutinga hatua ya nne ya mashindano hayo.


Akizungumza kwa hasira kali Vandenbroeck amesema kuwa amekuwa akiskia maneno kuhusu uwezo wa wachezaji wake pamoja na matokeo ambayo anayapata ndani ya uwanja akishinda hata akifungwa bado wanasema.


“Hatukuwa hapa nchini tulikuwa Nigeria hivi karibuni na tulishinda bao 1-0 ila watu walikuwa wanasema kuhusu wachezaji wangu pamoja na matokeo ambayo tunayapata.

“Sitaki kuona kwamba wachezaji wangu wanakosolewa kwani kwa asilimia kubwa wanajitoa na kufanya kazi kwa juhudi hilo lipo wazi.

“Haijalishi tunafungwa ama tunashinda bado hawastahili lawama iwe ni kwa mashabiki wale waliopo ndani ya timu pamoja na vyombo vya habari sitaki kuskia kuhusu wachezaji wangu wakilaumiwa nataka kulaumiwa mimi na kukosolewa iwe ni juu yangu,” amesema Sven.



YANGA IPO KAMILI GADO KUIVAA PRISONS MOROCCO KUMSAKA MBADALA WA ADAM SALAMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply