Home Uncategorized AZAM FC YASAKA MAJEMBE MENGINE MAWILI YA KAZI

AZAM FC YASAKA MAJEMBE MENGINE MAWILI YA KAZI


 KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amesema kuwa anahitaji kupata wachezaji wawili ama watatu ambao wataongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.


Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu kwa sasa kwenye msimamo inapambana kumsaka mshambuliaji mwingine ambapo inatajwa kuwa nyota wa FC Platinum, Perfect Chikwende yupo kwenye rada za kutua hapo.

Nyota huyo anakumbukwa na kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwa kumtungua kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mwalimu anahitaji kusajili wachezaji kati ya wawili ama watatu na timu lazima isajili kwa sababu ni timu kubwa.

“Sifa ya timu kubwa ni kufanya usajili nasi pia lazima tufanye usajili kwenye hili dirisha dogo, mashabiki wasiwe na mashaka ripoti inaeleza kila kitu.

“Ninadhani tutahitaji wachezaji wawili ambao watakuwa na kazi ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu ila kuhusu Perfect bado sijajua kama anahitajika na Azam FC,” .


Tayari Azam FC imepata saini ya nyota mmoja raia kutoka FC Lupopo, Mpiana Monzinzi.

SOMA NA HII  SAMATTA ATAKA MABAO 14 VILLA