Home Uncategorized OLE GUNNER ACHEKELEA KUCHEZA MECHI 9 BILA KUPOTEZA

OLE GUNNER ACHEKELEA KUCHEZA MECHI 9 BILA KUPOTEZA

 


OLE Gunner Solskjaer,  Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa wamecheza jumla ya mechi 9 bila kupoteza jambo linalowapa nguvu ya kufanya vizuri Kwenye mechi zao zijazo.


Ushindi wa bao 1-0 mbele ya Wolves,  Uwanja wa Old Trafford umewafanya United kufikisha jumla ya pointi 30 na kuwa nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 15.


Wapo nyuma ya Mabingwa watetezi Liverpool ambao wana pointi 32 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 15 msimu wa 2020/21.


 Mara ya mwisho Manchester United kupoteza ilikuwa ni Novemba Mosi walipofungwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal wakiwa nyumbani.

SOMA NA HII  DI MARIA ALIWAKA KWELI WAKATI PSG IKITINGA HATUA YA FAINALI