OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum kila kitu kipo sawa kwa upande wa maandalizi huku wakiwa wameomba kupewa kibali cha kuongeza idadi ya mashabiki.
Mara amesema Klabu ya Simba, imeliomba Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuwaongezea idadi ya watu kutoka 50% ya mashabiki kuingia uwanjani katika mechi dhidi ya Platinum ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Januari 6, 2021, Uwanja wa Mkapa.
Katika mechi dhidi ya Plateau, Caf iliwapa Simba nafasi ya kuingiza mashabiki 50% ya uwezo wa Uwanja wa Mkapa kwa hofu ya ugonjwa wa Covid 19.
Manara amesema kuwa wanataka zaidi ya idadi hiyo kutokana na hali ya Tanzania kiusalama wa afya ilivyo jambo ambalo limewafanya watume maombi ya kupewa kibali cha uongezeko la mashabiki zaidi.