Uncategorized

VIGONGO VIKALI VYA KUFUNGIA MWAKA 2020

admin December 31, 2020 4:47 am


LEO Desemba 31,2020 yamebaki  masaa kadhaa kwa Neema ya Mungu tuweze kufika mwaka mpya wa 2021.


Ndani ya Ligi Kuu Bara kuna mechi ambazo zitachezwa ikiwa ni za mwisho kwa mwaka 2020 kabla ya kuukaribisha mwaka mpya, mambo yatakuwa namna hii:-


Polisi Tanzania yenye pointi 23 inamenyana na Azam FC yenye pointi 29 ngoma inapigwa Uwanja wa Ushirika,Moshi.


Mchezo huu ni wa mzunguko wa pili, ule wa kwanza walipokutana Azam Complex, Polisi Tanzania ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Coastal Union ya Tanga yenye pointi 19 inamenyana na Namungo FC yenye pointi 17, ngoma inapigwa Mkwakwani.


Walipokutana Uwanja wa Majaliwa Coastal Union ilitunguliwa bao 1-0.


Tanzania Prisons yenye pointi 21 inamenyana na Yanga yenye pointi 43,ngoma inapigwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.


Uwanja wa Mkapa ngoma ilikuwa ni 1-1 baada ya dakika 90.

WATATU YANGA KUTOLEWA KWA MKOPO,WAWILI TAYARI MAMBO SAFI WILFRIED ZAHA AINGIA ANGA ZA AC MILAN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply