Uncategorized

COSTA MTATA KINOMA, KIDOGO AZICHAPE NA KOCHA

admin January 1, 2021 4:47 pm


 MWANDISHI wa habari nchini Hispania, Jose Ramon de la Morena amefichua kuwa ni bora Diego Costa ameamua kuondoka ndani ya Atletico Madrid.


 Ripota huyo amesema kuwa ilibaki kidogo achapane makonde na msaidizi wa kocha wake mkuu.

 

Inaelezwa kuwa mara baada ya kutokea kwa mzozo huo wa Costa na Nelson Vivas, ilibidi kocha mkuu Diego Simeone aingilie kati na kuamua ugomvi wao.


Taarifa zinaeleza kuwa kuanzia mwanzoni mwa msimu huu, Costa alikuwa njiani kuondoka kutokana na matatizo yake ya kifamilia, lakini kulikuwa na ugumu wa kuruhusiwa kuondoka.

 

Wakati mzozo wa mkataba wake ukiendelea, ndipo kuna siku alipishana kauli na msaidizi huyo na kilichotokea ilikuwa ni ugomvi mkubwa baina yao, lakini mwisho Costa alivunja mkataba na sasa ni mchezaji huru.

MTAMBO WA MABAO WAWAAMBIA YANGA IWEKE MKWANJA ASAINI KOCHA TANZANIA PRISONS: HAIKUWA MALENGO KUGAWANA POINTI MOJAMOJA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply