ADAM Adam, nyota wa JKT Tanzania ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na Chan anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Msimu wa 2020/21 aliwatungua Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex wakati JKT Tanzania ikifunga mabao 6-1.
Ndani ya JKT Tanzania ambayo imefunga jumla ya mabao 18 amehusika kwenye mabao nane akifunga saba na kutoa pasi moja ya bao.
Mzawa huyu chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed,’Bares’ hawa hapa walikutana na balaa lake:-
Bao 1, alifunga mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Mwadui FC aliwafunga mabao 3, Uwanja wa Mwadui.
Namungo FC,aliwafunga mabao 2 Uwanja wa Majaliwa na bao lake la saba alifunga mbele ya Biashara United kwa mkwaju wa penalti.