Uncategorized

WAPINZANI WA SIMBA WAIPIGA MKWARA KIMTINDO,WASEMA HAWAWAOGOPI

admin January 2, 2021 4:47 pm


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya FC Platinum Norman Mapeza amesema kuwa anawatambua wapinzani wake Simba vizuri hawampi presha atawasumbua ndani ya uwanja na kupata matokeo.


FC Platinum wametia timu leo Januari 2, Dar es Salaam na kupokelewa na uongozi wa timu hiyo ambao uliwahi mapema kuweka kambi ndani ya jiji la Dar es Salaam.


Kwenye mapokezi ya leo hakukuwa na mashabiki waliojitokeza wakiwa na jezi za rangi yoyote tofauti na mapokezi ya timu ya Plateua United.


Akizungumza na Saleh Jembe, Mapeza amesema kuwa wachezaji wapo vizuri na wanaamini watalinda ushindi na kupata ushindi ugenini.

“Tumekuja kwa kazi moja ya kutafuta ushindi hakuna jambo jingine ambalo tunahitaji hivyo wapinzani wetu wajiandae kisaikolojia tunawatambua, tunawaheshimu ila hatuwaogopi,” amesema.


Mchezo wa kwanza uliopita FC Platinum ilishinda bao 1-0 dhidi ya Simba Januari 6,Uwanja wa Mkapa ikiwa itashinda ama itapata sare inapenya hatua ya makundi.


Simba inatakiwa ishinde mabao zaidi ya mawili ili iweze kusonga hatua ya makundi.

ALIYEMPELEKA SIMBA MORRISON YAMKUTA YANGA YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply