Uncategorized

COASTAL YASAJILI KITASA KIPYA KUTOKA CONGO

admin January 9, 2021 9:47 am

 


KIRAKA Pascal Kitenge ambaye ni beki ndani ya uwanja amesaini dili la mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu ya Coastal Union ya Tanga.


Juma Mgunda ambaye ni Kocha Mkuu wa timu hiyo ameweka wazi kwamba malengo ya timu hiyo ni kuboresha safu ya ushambuliaji pamoja na ile ya ulinzi ambayo imekuwa ikipata tabu kupata matokeo ndani ya uwanja.

Kitenge, mwili jumba amesaini dili hilo akitokea Klabu ya AS Nyuki ya Congo na ametambulishwa rasmi leo Januari 9.


Kiraka mwingine ambaye yupo Coastal Union ni Ally Ally ambaye alikuwa anakipiga ndani ya KVZ ya Zanzibar na alicheza pia ndani ya Klabu ya Yanga, Edward Christopher, alikuwa anakipiga Ruvu Shooting yeye ni kiungo mshambuliaji.

KIPA HUYU MZAWA AINGIA ANGA ZA SIMBA NYOTA YANGA MTAMBO WA MABAO AOMBA KUSEPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply