Uncategorized

KOCHA SIMBA AIBUKIA MOROCCO BAADA YA KUBWAGA MANYANGA

admin January 9, 2021 11:47 am


KOCHA  Sven anatajwa kuibukia ndani ya Klabu ya F.A.R Rabat ya Morocco baada ya kubwaga manyanga ndani ya Klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo amesaini dili la miaka miwili kuifundisha timu hiyo baada ya kupata dili nono lililomfanya asepe ndani ya Simba.


 Vandenbroeck alikuja Bongo msimu wa 2019/20 kupokea mikoba ya Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi na mabosi wa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa alishindwa kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kutolewa na UD Songo hatua ya awali.


Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Simba Januari 6 kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kubwaga manyanga Januari 7 kwa kile alichoweka wazi kwamba ni masuala ya familia yalimuweka kando na timu hiyo.

WACHEZAJI TAIFA STARS WAFANYIWA VIPIMO ISHU YA CHAMA KUWA NGUMU KUBAKI NDANI YA SIMBA MSIMU UJAO IMEKAA HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply