LICHA ya nyota wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa kushindwa kucheza mchezo hata mmoja ndani ya Kombe la Mapinduzi kwa msimu wa 2021 amemshukuru Mungu kwa kukosa nafasi hiyo.
Mtibwa Sugar ambao walikuwa Mabingwa watetezi wa taji hilo, jana Januari 9 walivuliwa taji hilo baada ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba.
Kihimbwa hakuwa Kwenye kikosi kilichofungwa wala kile kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Chipukizi kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi.
Wakati kikosi chake kikipambana ndani ya Uwanja wa Amaan alikuwa akiendelea kutibu jeraha lake la mguu alilopata kabla ya mashindano kuanza.
Nyota huyo mzawa amesema:”Namshukuru Mungu kwa haya ninayopitia ninaamini kwamba haikuwa mpango wake nishiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ila nina amini kwamba kila kitu kitakuwa sawa.”
2019 chini ya Zuber Katwila ambaye kwa sasa yupo ndani ya Ihefu alikuwa sehemu ya kikosi kilichobeba taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.