Uncategorized

MKONGWE MORRIS AWATAJA WATAKAOVAA DARUGA ZAKE

admin January 12, 2021 12:47 pm


BEKI wa kati mkongwe Agrey Morris ambaye anakipiga ndani ya Klabu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina amesema kuwa hata akiweka daruga kabatini wapo watakaovaa.

Morris leo anastaafu kucheza ndani ya kikosi cha timu ya Tanzania, Taifa Stars rasmi ambapo kweye mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo utatumika pia kumuaga nyota huyo.

Mchezaji huyo amesema: “Nina amini wapo wenye uwezo wa kuvaa viatu vyangu na mimi pia kwa sasa umri umesogea hivyo najiweka kando kidogo, vijana wanakuja kwa kasi ukiangalia kuna Sebo, Ame na Mwamnyeto kwa hiyo huu ni muda wangu sahihi.

“Kwa upande wa Azam FC nitastaafu msimu wa 2022 nikimaliza mkataba wangu huu wa miaka miwili. Kwa kuwa tayari nimeshamaliza huku ndani ya Stars nikimaliza mkataba ndani ya Azam FC nitakuwa pembeni” .


KOCHA YANGA ALITAKA KOMBE LA MAPINDUZI KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA DR CONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply