Yanga SC

FISTON APEWA MAJUKUMU MAKUBWA, MKATABA WAKE WAZUA GUMZO

admin January 19, 2021 5:47 am


WAKATI ishu ya mkataba wake ukiibua gumzo kuhusu uhalali wake wa kusaini miaka miwili ama miezi sita, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa kazi mpya ya mshambuliaji wake Fiston Abdoul Razak ambaye ni mshambuliaji ni kufunga mabao mengi ili kuipa timu hiyo ushindi.

Kaze amesema kuwa mshambuliaji huyo anamtambua vema na anaamini kwamba anaweza kufanya makubwa ndani ya kikosi hicho.

Razak ambaye ni raia wa Burundi anaungana ndani ya kikosi cha Yanga ambacho yupo mshikaji wake wa kitambo, Saido Ntibanzonkiza ambaye ni raia wa Burundi.

Kaze amesema kuwa:”Kazi kubwa ya Fiston itakuwa ni kwenye kufunga na hilo sina mashaka nalo juu yake kwa sababu ni mchezaji mzuri na anajua kufanya kazi yake kwa umakini.

“Kwa muda tumekuwa tukifanya vizuri ndani ya uwanja ila tatizo lilikuwa kwenye umaliziaji wa nafasi zinazotengenezwa pamoja na namna ya kutengeneza nafasi zenyewe.

“Ujio wake ndani ya kikosi utakuwa ni furaha kwetu na mashabiki kiujumla ni suala la kusubiri na kuona kwa kuwa kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imecheza jumla ya mechi 18 kibindoni ina pointi 44.

Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 29 huku ile ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao saba.

Mkataba wa Fiston umekuwa unaleta utata ambapo mchezaji mwenyewe anasema kwamba amesaini dili la miezi sita huku mabosi wa Yanga wakieleza kuwa amesaini dili la miaka miwili.

BAADA YA CHIKWENDE, MAJEMBE HAYA MATANO YAPO KWENYE HESABU ZA SIMBA MTAMBO WA MABAO AZAM WAPANIA KUENDELEA KUCHEKA NA NYAVU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply