Taifa Stars

KOCHA ZAMBIA ATOA KAULI YA KIBABE AKIIVAA TANZANIA

admin January 19, 2021 2:47 pm

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Zambia, Sredojevic Milutin Micho amekiri kwamba anatarajia kukutana na mchezo mgumu dhidi ya Taifa Stars leo.

Zambia leo itacheza dhidi ya Taifa Stars kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi D la michuano ya CHAN, mchezo utakaopigwa jijini Limbe, Cameroon majira ya saa 1:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Akizungumzia mchezo huo Micho amesema: “Tunaiheshimu Tanzania kwakuwa najua wana ligi ya ndani nzuri na imara, najua ubora wao mpaka kufikia hapa ila tumejiandaa kupambana nao leo hii,”

Hizi ni fainali za tatu kwa Micho ambaye amewahi kupita kwenye kikosi cha klabu ya Yanga, ambapo fainali mbili za kwanza alikuwa akikiongoza kikosi cha Uganda mwaka 2014 na 2016.

MASTAA HAWA KAZI WANAYO HILI HAPA JESHI LA STARS LITAKALOIVAA ZAMBIA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply