Home Yanga SC MUANGOLA WA YANGA MAMBO BADO KIKOSINI

MUANGOLA WA YANGA MAMBO BADO KIKOSINI

MATUMAINI ya mtambo wa mabao ndani ya Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola kurejea ndani ya uwanja kwa sasa ni hafifu kwa kuwa bado yupo kwenye matibabu.

Nyota huyo alitonesha maumivu yake ya nyonga ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wakati wakishinda mabao 2-1.

Alipanda boti mpaka visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi ila alirejeshwa fasta Dar ili kuendelea na matibabu baada ya kujitonesha mazoezini.

Yanga ikiwa imefunga mabao 29, Muangola huyo amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao manne.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa bado anaendelea na matibabu ya nyonga hivyo akiwa fiti itajulikana muda wake wa kurejea uwanjani.

“Bado kwa sasa Carlinhos anaendelea na matibabu hivyo akipona itafahamika anaweza kurejea lini uwanjani ndani ya uwanja,” amesema.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKITAMBA NA MUSONDA....WAPINZANI WAO CAF WASHUSHA MAJEMBE YA KAZI...NI BALAA TUPU..