Simba SC

DALALI WA SIMBA AITWA TFF

admin January 21, 2021 1:47 pm

 

KUFUATIA kuikatia rufaa kamati ya uchaguzi ya Klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Boniface Lihamwike kwa muda wa siku 20 sasa, kupinga jina lake kukatwa katika kinyangan’yilo cha kuwania uenyekiti, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekuita Hassan Dalali ili kuweza kuanza mchakato wa kusikiliza rufaa yake hiyo. 

Dalali aliikatia rufaa kamati ya uchaguzi ya Simba kwenda TFF kupinga kukatwa jina lake katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa klabu hiyo unaotarajia kufanyika Februari 7 kufuatia aliyekuwa mwenyekiti wa nafasi hiyo, Swed Mkwabi kujiuzuru Septemba mwaka juzi kutokana na sababu zake binafsi.

Aidha kamati hiyo tayari imeshafungua kampeni iliyoanza Jumapili iliyopitan huku ikiwa inadumu dani ya siku 21 ikiw ana wagombea wawili Juma Nkamia na Mutaza Mangungu huku watatu kati yao Hamisi Omari Tika, Rashid  Shangazi na Anton Mwakisu wakijitoa dakika za mwisho. 

Akizungumzia wito huo Dalali amesema: “TFF wameshaniita kupitia kwa katibu mkuu Kidau ambaye alinipigia simu na kunitaka niwasilishe kopi ya rufaa yangu na tayari nimeshafanya hivyo na ameshanieleza ndani ya wiki hii inaweza kusikilizwa,” 

NTIBAZONKIZA AWEKWA MTEGONI YANGA RASMI, MKUDE AJITOKEZA HADHARANI NA KUOMBA MSAMAHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply