Simba SC

RASMI, MKUDE AJITOKEZA HADHARANI NA KUOMBA MSAMAHA

admin January 21, 2021 2:47 pm


KIUNGO mkabaji wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amejitokeza rasmi na kuomba radhi kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizokuwa zikimkabili.

Mkude ambaye ni mchezaji Mwandamizi wa kikosi cha Simba hajaichezea Simba tangu  Desemba 23, mwaka jana alipocheza mchezo wa michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Akiomba radhi hiyo Mkude amesema: “Tumeumbwa kukosea lakini haimaanishi nitakosea tena, mimi ni Mwanasimba mwenzenu na klabu hii ni sehemu ya maisha yangu.

“Naamini wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki mtanielewa na kunisamehe,”

DALALI WA SIMBA AITWA TFF MKUDE : TUMEUMBIWA KUKOSEA..SITAKOSEA TENA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply