Home Yanga SC ISHU ILIYOMUONDOA MWAMBUSI YANGA HII HAPA

ISHU ILIYOMUONDOA MWAMBUSI YANGA HII HAPA


IMEBAINIKA kuwa sababu iliyomuondoa aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Yanga, Juma Mwambusi ni matatizo ya jino.

Mwambusi alitangaza uamuzi huo Januari 21, mwaka huu ambapo aliwasilisha barua kwa uongozi akiomba kupumzika na kutumia muda huo kwa ajili ya matibabu.

Mwambusi alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akiwa kama kocha msaidizi wa Mserbia, Zlatko Krimpotic ambaye baadaye alifutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Mrundi Cedric Kaze.

Akiwa na kikosi cha Yanga mwambusi alihudumu kama kocha msaidizi kwenye michezo 18 ya ligi na kufanikiwa kushinda michezo 13 huku wakitoa sare michezo mitano.

Akizungumzia kuhusu afya yake Mwambusi alisema: “Ushauri wa Daktari ndiyo umesema nipumzike, wiki inayokuja ndiyo nitaenda kufanyiwa upasuaji Muhimbili ili kuondoa jino zima lakini kwa sasa nimeanza matibabu madogo madogo, naomba Watanzania waniombee,” 

SOMA NA HII  UNAIKUMBUKA ILE 'MOMENTI' YA AZIZ KI KUSHANGILIA NA MAKAMBO JUZI...BASI KUMBE NYUMA YA PAZIA KUNA HILI KATI YAO...