Home Simba SC KUMBE LWANGA SIMBA BADO SANA

KUMBE LWANGA SIMBA BADO SANA

 BONIFACE Pawasa, beki mkongwe aliyecheza ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa bado kiungo Thadeo Lwanga anahitaji muda ili kuweza kuwa bora kwa kuwa ameonekana hayupo fiti.

Lwanga raia wa Uganda amesaini dili la miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba na alianza kuonyesha makeke yake kwenye Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar ambapo walimaliza wakiwa nafasi ya pili baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Usajili wake umezua gumzo baada ya jina lake kupigwa panga kwenye orodha ya wale ambao wamesajiliwa na Simba ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).

Kuhusu hilo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzale amesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka nyota huyo ni mali yao.

Pawasa amesema kuwa anawajua wachezaji wengi ambao wanatoka Uganda huwa wanakuwa fiti ndani ya uwanja ila kwa namna alivyomuona Lwanga, bado sana.

“Bado sana kwa sasa hajaweza kuonekana fiti, asili ya wachezaji wanaotoka Uganda huwa wanakuwa na nguvu nyingi pamoja na uwezo mkubwa ndani ya uwanja.Kwa kiungo mkabaji ni mhimili wa ushindi ndani ya timu sasa Simba inahitaji mkabaji kweli.

“Kwa namna ambavyo nimemuona Lwanga kwenye Kombe la Mapinduzi anatakiwa kuongeza juhudi ili kufikia ile hatua ya ubora wake, labda kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kumemfanya awe hivyo ila ni lazima aongeze kiwango zaidi,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA WA NEYMAR, COUNTINHO NA CASEMIRO AJITOSA UKOCHA MKUU SIMBA...UONGOZI WASISITIZA SIFA..