Home Simba SC MRITHI WA SVEN VANDENBROECK SIMBA AANZA KAZI RASMI LEO

MRITHI WA SVEN VANDENBROECK SIMBA AANZA KAZI RASMI LEO


 IKIWA leo Januari 24 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamemtambulisha mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba ameanza kazi rasmi.

Mrithi wa Sven ni Didier Gomes Da Rosa ambaye ametua Bongo leo na kusaini dili la miaka miwili ametambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez akiwa sambamba na mpiga mgenga, Haji Manara ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari.

 Didier Gomes Da Rosa ambaye ni raia wa Ufaransa amekanyaga kwa mara ya kwanza Uwanja wa mazoezi wa Klabu ya Simba wa Mo Simba Arena.

Anaanza kukinoa kikosi hicho ambacho kimetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na mchora ramani alikuwa ni Sven ambaye kwa sasa yupo zake ndani ya kikosi cha FAR Rabat ya Morroco.

Atafanya kazi kwa ushirikiano na mzawa, Seleman Matola ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyopo nchini Cameroon kwa ajili ya kushiriki michuano ya Chan.


SOMA NA HII  KWA SIMBA HII...MTENDAJI MKUU MPYA ATATOBOA KWELI...?...BARBARA KAMWACHIA SWALI ZITO...