Simba SC

HAWA HAPA NYOTA NANE HAWAJAANZA MAZOEZI SIMBA

admin January 26, 2021 9:47 am


IKIWA tayari Klabu ya Simba imeanza maandalizi ya Simba Super Cup baadhi ya wachezaji bado hawajaanza mazoezi na timu kutokana na sababu mbalimbali.

Hawa hapa nane bado hawajaanza kufanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes:-Erasto Nyoni anasumbuliwa na majeraha alikuwa na timu ya Taifa ya Tanzania ila amerejeshwa Bongo kuendelea na matibabu.

Pascal Wawa alikuwa kwenye mapumziko mafupi pia alikuwa anaumwa wakati anaanza mapumziko wakati ule wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Jonas Mkude ana adhabu yake kutokana na matatizo ya nidhamu.

Joash Onyango alikuwa kwenye mapumziko.

Aishi Manula yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Cameroon.

Luis Miquissone alipewa mapumziko.

Said Ndemla yupo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Cameroon pamoja na Ibrahim Ame.

YANGA KUMSHUSHA MSHAMBULIAJI WAO MWILI JUMBA MUDA WOWOTE AZAM FC WAPO TAYARI KWA MZUNGUKO WA PILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply