Home Azam FC KOCHA AZAM FC ATAJA SABABU ZA KUMTUMIA KIPA NAMBA NNE

KOCHA AZAM FC ATAJA SABABU ZA KUMTUMIA KIPA NAMBA NNE

 


GEORGE Lwandamina,Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa ataendelea kumtumia kipa namba nne wa kikosi hicho ili aweze kujenga hali ya kujiamini.

Wilbol Maseke ni kipa namba nne ndani ya kikosi cha Azam FC ambapo aliweza kuonekana vema kwenye Kombe la Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.

Mabingwa hao wa kihistoria wa Kombe la Mapinduzi wakiwa wameutwaa ubingwa mara tano waliishia hatua ya nusu fainali baada ya kutolewa na Yanga ambao ni mabingwa kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga, Maseke alianza kikosi cha kwanza na alifungwa bao moja kabla ya mpira kuisha alitolewa dakika za lala salama na nafasi yake ikachukuliwa na kipa Benedict Haule.

Makipa wengine wa Azam FC ni pamoja na David Kissu ambaye ni kipa namba moja na Mathias Kigoya ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi.

Lwandamina amesema:”Maseke  ni kipa mzuri bado nitaendelea kumpa nafasi kikosi cha kwanza ili aweze kujenga hali ya kujiamini, “.


SOMA NA HII  JINA LA KIUNGO AZAM FC LAONDOLEWA STARS, MBADALA WAKE HUYU HAPA