Home news PAMBANO LA IBRA CLASS NA MWALE WA ZAMBIA MAMBO NI MOTO

PAMBANO LA IBRA CLASS NA MWALE WA ZAMBIA MAMBO NI MOTO


 BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema kuwa itatumia pambano la bondia Ibrahim Class na Dennis Mwale wa Zambia (Rhumbo in Dar) kuutangaza utalii wa nchi nje ya mipaka yake.

Bondia wa Tanzania, Class na Mwale watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena wa Masaki kuwania ubingwa wa mabara wa WBF wa uzito wa Super Feather.

Pambano hilo limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports na litaonyeshwa nchi zaidi ya 150 duniani.  Siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine nane yalishirikisha mabondia mbalimbali ikiwa pamoja na bondia nyota wa Bulgaria, Tervel Pulev ambaye amewasili pamoja na bondia nyota wa uzito wa juu duniani Kubrat Pulev ambaye alipigana na Anthony Joshua mwishoni mwa kwaka jana.

Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Mindi Kasiga amesema jana kuwa watatumia fursa hiyo kuutangaza utalii wa nchi kwani mapambano ya ngumi hayo yataonekana nchi nyingi.

“Hii ni fursa kwetu kuutangaza utalii na kuingia kusapoti Jackson Group Sports,” amesema Kasiga.

Mbali ya TTB, pambano hilo limedhaminiwa na benki ya CRDB ambapo meneja wa chapa, Joe Bendera amesema kuwa wanazidi kuendeleza michezo nchini kwani walidhamini pia mpira wa kikapu, kuandaa marathoni na kutoa fursa ya masomo kwa vijana 26 kupitia mpira wa kikapu.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Boxing Stars (GBS), Scott Farrell amesema kuwa wamevutiwa na kampuni ya Jackson Group Sports na kuamua kufanya nao kazi pamoja kuinua mchezo wa ngumi za kulipwa.

Amesema kuwa  lengo lao ni kuinua vipaji vya mchezo huo hapa nchini. Mbali ya wadhamini hao, wadhamini wengine ni Azam TV, Onomo Hotel, Precision Air, Vitasa, Bono 5, Hotel Demag na Henessy.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na mabondia wote wamewasili kwa ajili ya kuzichapa Ijumaa.

SOMA NA HII  BAADA YA KIMYA KIREFU....MZEE KILOMONI AIBUKA NA HILI JIPYA KWA SIMBA....AMPA MAAGIZO MO DEWJI...