UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao mpya Fiston Abdulazack ambaye wamempachika jina la mtambo wa mabao amekuja kufanya kazi itakayowapa furaha wana Jangwani.
Nyota huyo ametua Bongo jana, Januari 29 akitokea nchini Burundi na amesaini dili la miezi sita ambalo lina kipengele cha kuongeza mkataba.
Anaungana na rafikiye, Said Ntibanzokiza ambaye alianza kazi ndani ya Yanga akiwa amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara.
Ntibanzokiza na rai wa Burundi na alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa ni mchezaji huru na alikuwa anakipiga kwenye timu ya Taifa ya Burundi.
Alianza kufunga bao lake la kwanza mbele ya Dodoma Jij, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na alifunga bao la pili mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.
Ofisa Uhamasishaji ndani ya kikosi cha Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kazi yake ni kuwapa furaha wanajangwani na kutuma salamu kwa wapinzani wao.
“Amekuja ndani ya Yanga kufanya kazi ya kuwapa furaha mashabiki wa Yanga ambao kwa sasa ni muda wao wa kutamba na kufurahi.
“Malengo yetu ni kuona kwamba tunachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na lile Kombe la Shirikisho, tumeanza na lile la Mapinduzi hivyo kuna mengine yanakuja zaidi,” .
Nyota huyo amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya kikosi cha Yanga hivyo matumaini yake ni kufanya vizuri na kutimiza kile ambacho mashabiki wanahitaji.