Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

KUHUSU DILI LA KIPA MPYA SIMBA.. UKWELI WOTE A-Z HUU HAPA…

admin August 11, 2023 9:32 pm

Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano ya kuinasa saini ya Mlinda Lango, Ayoub Lakred aliyekuwa akiichezea timu ya FAR Rabat ya nchini Morocco inayonolewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Young Africans, Nasreddine Nabi.

Chanzo Makini kutoka ndani ya Simba SC kimeeleza kuwa, makubaliano ya pande hizo mbili yamefikiwa ikiwa ni siku chache tangu kuachana na Malinda Lango kutoka nchini Brazili, Jefferson Luis aliyeondolewa kambini nchini Uturuki kutokana na majeraha ya misuli.

“Ni kweli yupo nchini na maongezi hadi sasa yanaendelea vizuri, ni matumaini yetu atakuwa msaada mkubwa kutokana na ushiriki wetu wa mashindano mengi ya ndani na kimataifa,” kimeeleza chanzo hicho.

Lakred mwenye umri wa miaka 28, alichezea FAR Rabat, timu nyingine aliyowahi kuichezea ni RS Berkane.

Usajili wa Lakred unakuwa ni wa pili kwa Mlinda Lango ndani ya kikosi cha Simba SC.

KUHUSU ILE ISHU YA FEI TOTO KUIPIGA CHINI YANGA…ALLY KAMWE LEO KAIBUKA NA HILI JIPYA… BAADA YA KUICHAPA KWA MBINDE SINGIDA JANA…AHMED ALLY KAJA NA HILI JIPYA KWA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply