BARAZA la Michezo Tanzania (BMT), leo linatarajiwa kusimamia uchaguzi mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT).
Uchaguzi huo ni wa kikatiba na unatarajiwa kujaza nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa RT, Ombeni Mzavara amesema: โMaandalizi yote ya uchaguzi mkuu wa chama cha riadha Tanzania yamekamilika.
โKwa mwaka huu tunatarajia uchaguzi huu utasimamiwa na BMT, ambao wamehusishwa katika mchakato mzima wa uchaguzi tangu utaratibu wa kuchukua na kurudisha fomu,โ