Home Azam FC ALIYEMTULIZA KAGERE ATOA KAULI YA KIBABE

ALIYEMTULIZA KAGERE ATOA KAULI YA KIBABE

 BAADA ya kurejea uwanjani na kufanikiwa kuhusika katika mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata Azam dhidi ya Mlandege mshambuliaji wa Azam, Prince Dube ametamba kuwa ataendelea kufunga kama ambavyo aliuanza msimu huu.

Dube alikuwa nje ya Uwanja tangu Novemba 25, mwaka jana baada ya kuvunjika mkono wake wa kushoto kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, Jijini Dar es Salaam. 

Kabla ya kupata majeraha hayo Dube alikuwa tayari amehusika kwenye mabao 10 ya Azam kwenye Ligi Kuu Bara akifunga mabao sita na kuasisti mara nne kiasi cha kumkalisha Kagere ambaye alikuwa na mabao manne pekee wakati huo. 

Akizungumzia matarajio yake baada ya kurejea uwanjani Dube amesema: “Kwanza niseme namshukuru Mungu kwa kurejea tena uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya kuvunjika mkono niliyoyapata mwezi Novemba mwaka jana.

“Lakini pia nawashukuru wale wote ambao walikuwa sehemu ya matibabu yangu na kufanikisha mimi kurejea tena uwanjani. 

“Niliahidi kwamba nitarejea uwanjani nikiwa bora zaidi na nafurahi kuona nimefanikiwa kuhusika kwenye mabao mawili tuliyoyapata dhidi ya Mlandege licha ya kwamba tulipoteza mchezo uliofuata dhidi ya KMKM.

“Naamini nitarejea tena kwenye kasi yangu ya ufungaji kama ambavyo ilikuwa mwanzoni mwa msimu huu, hivyo Kama nilivyoahidi ya kwamba nitarejea uwanjani nikiwa bora zaidi ndicho ambacho nitakifanya,” 

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM...FEI TOTO AFUNGUKA ISHU YAKE NA RAIS SAMIA...AITAJA YANGA...