Home Ligi Kuu BEKI ALIYEKUWA ANAWINDWA YANGA, APEWA JEZI YA NTIBANZOKIZA

BEKI ALIYEKUWA ANAWINDWA YANGA, APEWA JEZI YA NTIBANZOKIZA


 BEKI mzawa mwenye uwezo wa kupiga mipira iliyokufa pamoja na kufunga akiwa nje ya 18 amemalizana na mabosi wa Ruvu Shooting kwa dili la miezi sita akitokea Klabu ya Namungo.

Beki huyo aliwekwa kwenye rada za Yanga kabla ya kuambulia patupu na kumnasa beki wa kati kutoka Mtibwa Sugar, Dickson Job.

Yanga inayonolewa na Cedric kaze awali ilikuwa kwenye mazungumzo na beki huyo ambapo alikwama kutua ndani ya timu hiyo baada ya mabosi wake kushindwana kwenye maslahi na kwa sasa atakuwa ndani ya Ruvu Shooting.

Manyama aliwahi kucheza ndani ya Yanga na pia alicheza ndani ya Ruvu Shooting hivyo amerejea nyumbani ambapo awali aliweka wazi kwamba anapenda kucheza hapo kwa kuwa ni sehemu bora kwake.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa mchezaji huyo anajiunga na timu bora kuongeza uimara ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Charles Mkwasa.

“Amekuja kwenye kikosi bora kuendelea ubora wake kwa kuwa yeye yupo vizuri, naona kwamba atazidi kuwa imara ndani ya uwanja ni suala la kusubiri.

“Jezi ambayo amechagua na itakuwa mali yake ndani ya Ruvu Shooting itakuwa ni namba 60 kwa kuwa ameichagua mwenyewe,” amesema.

Jezi hiyo ndani ya Klabu ya Yanga inavaliwa na nyota wao Saido Ntibanzokiza ambaye ni ingizo jipya kutoka Burundi.

Akiwa ndani ya Namungo inayoshiriki Kombe la Shirikisho aliwahi kuwatungua Azam FC kwa mpira wa adhabu akiwa nje ya 18 kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.

SOMA NA HII  LIGI KUU BARA KADI 600 ZATOLEWA...MGUNDA AMKANA KANOUTE..."NAMUONYA SANA HASIKII