Home Yanga SC JEMBE JIPYA YANGA KUTUA ALHAMISI

JEMBE JIPYA YANGA KUTUA ALHAMISI

 


MSHAMBULIAJI mpya wa klabui ya Yanga, Fiston Abdoul Razak anatarajiwa kutia nchini siku ya Alhamisi ili kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Fiston ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogop ambao wanakuja kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachopambana kushinda tajui la Ligi Kuu msimu huu.

Kikosi cha klabu ya Yanga kimeanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na michezo ya mzunguko wa pili jana Jumatatu, mazoezi yanayofanyika kwenye kambi yao ya Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ambapo imejikusanyia pointi 44 katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa.

SOMA NA HII  YANGA YA GSM WAZIDI KUTAKATA MSIMU HUU...WAIACHA KWENYE MATAA SIMBA YA MO DEWJI KWENYE KILA KONA...