Home Simba SC JESHI LA SIMBA KUREJEA KAMBINI JUMATATU

JESHI LA SIMBA KUREJEA KAMBINI JUMATATU


KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, klabu ya Simba kinatarajiwa kurejea rasmi kambini Januari 25, ambayo ni siku ya Jumatatu ya wiki Ijayo.

Tangu kumalizika kwa michuano ya kombe la Mapinduzi, kikosi cha Simba iliyopoteza fainali ya michuano hiyo mbele ya Yanga kimekuwa kwenye mapumziko.

Inatajwa kuwa siku hiyo Simba inaweza kuanza rasmi mazoezi na kocha wake mpya ambaye yuko kwenye mchakato wa kutangazwa hivi karibuni, ili kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inatarajiwa kuanza kibarua chake kwenye Ligi ya mabingwa Afrika Februari 12, mwaka huu dhidi ya AS Vita kutoka DR Congo. 

SOMA NA HII  ACHANA NA MASTAA WAPYA....MAKOCHA WAPYA WATAKAO MSAIDIA MBRAZILI SIMBA HAWA HAPA..