Home Uncategorized MGOGORO WA ZIDANE NA BALE KUSHUSHA THAMANI YA MCHEZAJI

MGOGORO WA ZIDANE NA BALE KUSHUSHA THAMANI YA MCHEZAJI


MGOGORO unaoendelea kati ya Meneja wa Real Madrid  Zinedine Zidane na mchezaji wake Gareth Bale umeelezwa kuwa unaidumisha thamani ya nyota huyo.

Zidane hivi karibuni alilipotiwa akimwambia mchezaji wake kuwa haitajiki ndani ya klabu hiyo na anapaswa kuondoka kwani hana nafasi.
Bale ambaye inatajwa kuwa kuna timu moja nchini China ambayo inamhitaji na inataka kumfanya awe mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu inadaiwa imeanza kufifisha matumaini ya kumpata nyota huyo.
Rais wa Madrid, Florentino Perez imeripotiwa hakuwa na furaha kwani hapendi kuona migogoro ndani ya timu hiyo kwa kuwa anaamini itashusha thamani ya mchezaji wake na suala zima la kumpeleka nchini China linatazamiwa kuwa la malipo ya kodi nyingi.
SOMA NA HII  YANGA YAKUBWA NA MSALA, MAKOMANDOO WAJIONDOA, WAANDIKA BARUA, IDADI KAMILI HII HAPA