Home Habar za Usajili Simba KUHUSU KOCHA MPYA SIMBA…KOCHA WA KAIZER CHIEFS AFUNGUKA ALICHOKITETA NA BARBARA…”BADO SIJAAMUA”…

KUHUSU KOCHA MPYA SIMBA…KOCHA WA KAIZER CHIEFS AFUNGUKA ALICHOKITETA NA BARBARA…”BADO SIJAAMUA”…


Taarifa za kuaminika zinasema aliyekuwa kocha wa Kaizer Chiefs na kutimuliwa kabla ya mkataba wake kuisha Stuart Baxter raia wa Uingereza (68), April 24, 2022 alifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Baxter anayehusishwa kuchukua mikoba ya Pablo alikutana na Barbara jijini Johannesburg Simba ilipoenda kucheza na Orlando Pirates mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kocha huyo amesema kikao hicho kilikuwa tu kwa ajili ya maendeleo ya timu hiyo.

“Nilikuwa na mazungumzo kadhaa ndani ya nchi katika Ligi Kuu ya Soka na barani, ikiwa ni pamoja na kukutana na Simba,” Baxter sasa ameiambia SABC Sport,

“Lakini nadhani ni muhimu kusahihisha habari fulani potofu. Nilichukua kikao na Simba kujadili mipango yao kwenda mbele na ninahisi sasa kuna mawakala wanaopotosha umma kuhusu kilichojadiliwa.

“Bado sijaamua kama kutakuwa na mazungumzo zaidi na klabu yoyote ambayo nimekutana nayo. Lakini mpira wa miguu ni wakati, kwa hivyo tusubiri tuone.”

Muingereza huyo aliachana na Amakhosi mwezi Aprili wakati bado alikuwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Simba kwa sasa ipo chini ya kocha Msaidizi Seleman Matola baada ya kutimuliwa kwa Pablo Franco ambaye alishindwa kufikia malengo aliyowekewa na klabu hiyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA SIMBA..KAZE AVUNJA UKIMYA YANGA....JULIO AKUBALI YAISHE..ADAI YANGA NI BABA LAO...