Home Simba SC MORRISON ANG’ARA, SIMBA IKIUA 4-1 DHIDI YA WASUDANI

MORRISON ANG’ARA, SIMBA IKIUA 4-1 DHIDI YA WASUDANI


Mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Simba Super Cup kati ya Simba na Al Hilal umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-1.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya bao 1-1 mabao yaliyofungwa na Rally Bwalya kwa upande wa dakika ya 38 na Salim Mohamed kwa upande wa Al Hilal aliyefunga dakika ya 44.

Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi na dakika ya 52 Al Hilal walikosa bao baada ya mshambuliaji wa Hilal kupiga shuti langoni lililookolewa na Beno Kakolanya.

Simba nao dakika ya 54 walijibu mapigo kupitia kwa Chama ambaye alipiga shuti kali lililopanguliwa na mlinda lango wa Al Hilal.

 Dakika ya 60 Al Hilal walifanya mabadiliko ya wachezaji wawili sambamba na Simba waliowatoaFrancis Kahata na Meddie Kagere na nafasi zao kuchukuliwa na Benard Morrison na Chriss Mugalu.

Katika mechi hiyo baadhi ya wachezaji wa Al Hilal katika mchezo huo walionekana kutokuwa fiti kimwili kwani mara kwa mara walionekana kubanwa na misuli kwa zaidi ya mara moja.

Dakika ya 69 Simba walikosa bao la wazi baada ya Morrison kufanya kazi nzuri na kuoiga pasi kwa Chriss Mugalu ambaye alipiga mpira uliodakwa na golikipa wa Hilal.


Dakika ya 70 Al Hilal walifanya mabadiliko mengine ya wachezaji wawili ambao dakika mbili baada ya kuingia Simba walipata bao kupitia kwa nyota wao mpya Chikwende aliyepasi mpira nyavuni baada ya kipa wa Hilal kupangua shuti kali lililokuwa limepigwa na Morrison.

Dakika ya 73 Simba waliwatoa Clatous Chama na Perfect Chikwende na nafasi zao kuchukuliwa na Ibrahim Ajib na Miraji Athuman.

Pia dakika ya 77 samba mshambuliaji wa Al Hilal alikosa bao la wazi akiwa amebaki yeye na golikipa na kupiga nje kidogo ya lango la Simba.

Dakika ya 80 kocha mkuu wa Simba Didier Gomez alimtoa nje kiungo Taddeo Lwanga na nafasi yake kuchukuliwa na Muzamiru Yassin.

Dakika ya 86 Benard Morrison aliwapatia Simba bao la tatu kwa shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Al Hilal na kuzama nyavuni.

SOMA NA HII  KWA HIZI HESABU ZA BENCHIKHA SIJUI KAMA ANATOKA MTU KWA MKAPA

Baada ya bao hilo uwanja mzima ulilindima kumshangilia Morrisson aliyeshangilia kwa kuweka mpira ndani ya bukta na kuanza ktembea kwa madaha.

Yule yule Morrison dakika ya 87 alipiga msumari wa mwisho kwa kufunga bao lake la pili na la nne kwa timu hali iliyoamsha shangwe nyingi uwanjani hapo zilizodumu mpaka mpira unamalizika.


Bwalya pia ameibuka mchezaji bora wa mechi hiyo na amepata zawadi ya Sh 500,000.