Home Habari za michezo KWA HIZI HESABU ZA BENCHIKHA SIJUI KAMA ANATOKA MTU KWA MKAPA

KWA HIZI HESABU ZA BENCHIKHA SIJUI KAMA ANATOKA MTU KWA MKAPA

Kocha Mpya wa Simba

KOCHA mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amepiga hesabu kali kuelekea katika mchezo wao ujao wa hatua ya makundi dhidi ya Wydad ya Morocco kwa kuwabadilishia program ya mazoezi mastaa wa timu hiyo kwa wapigisha mazoezi kwa siku mara mbili kutokana na ratiba ngumi ya michezo iliokuwa mbele yao.

Katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika leo  asubuhi kocha huyo alianza kuwapa program kwa wachezaji ambao hawakucheza na wale waliocheza dakika chache kwenye mchezo  na Wydad Casablanca na jioni wakajumuishwa wachezaji wote, uwanja wa Mo Arena ulipo Bunju, Dar es Salaam.

Benchikha amefikia hatua hiyo kuelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar unaotarajia kupigwa Desemba 15, mwaka huu kabla ya kuelekea katika mchezo  Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Desemba 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Benchikha amesema  kwa sasa wamekuwa katika kipindi kigumu cha michezo yao iliokuwa mbele yao, wanahitaji kufanya maandalizi mara mbili zaidi ya ratiba zao zilizokuwepo awali.

Amesema kikubwa anahitaji wachezaji wake kuwa fiti na kuwaanda kisaikolojia, kiufundi na kimbinu na kutumia siku  zilizosalia kuendelea kukisuka kikosi chake kinakuwa imara zaidi na kuendelea kuonyesha mabadiliko ndani ya uwanja.

“Tuna michezo miwili mikubwa ambayo ipo mbele yetu  kiukweli yote tunahitaji kuona tunapata matokeo makubwa ili kujiweka sawa na maeneo ambayo tupo, ukianzia kwenye ligi nafasi ambayo tupo na hali ambayo tupo nayo kwa sasa lazima tufanye mabadiliko makubwa katika program zetu.

Nataka mazoezi zaidi  kwa muda l tumebakia nao angalau mara mbili kwa siku na kila mchezaji anatapaswa kujitoa katika uwanja wa mazoezi kwa sababu mchezo wetu na Kagera naamini utakuwa mgumu kama utakavyokuwa mchezo wetu na Wydad,” amesema Benchikha.

SOMA NA HII  AISEE!! NABI AZINYAKA SIRI ZA INONGA...AWAKABIDHI MAYELE NA MUSONDA...ISHU NZIMA HII HAPA A-Z