Home Simba SC MRITHI WA SVEN KUTAJWA RASMI NDANI YA SIMBA

MRITHI WA SVEN KUTAJWA RASMI NDANI YA SIMBA

 


UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa kabla ya mashindani ambayo wameyatambulisha ya SIMBA INTER CUP ambayo yatashirikisha timu tatu hayajaanza watakuwa wameshamtambulisha kocha mpya.

Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba alibwaga manyanga Januari 7 muda mfupi baada ya kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi kwa udhindi wa mabao 4-0.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzale amesema timu tatu zitashiriki ambazo ni Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan. Mashindano yataanza Januari 27 hadi 31, 2021

“Kabla ya mashindano kuanza tutakuwa tumeshamtangaza kocha mpya hivyo kesho mashabiki watamjua kocho mpya wa Simba wasiwe na mashaka,” amesema Gonzale.

SOMA NA HII  FAILI LA MASTAA WAPYA NA WATAKAO TEMWA SIMBA HILI HAPA....MBRAZILI 'KAKAZA SHINGO' AISEE..