Home Simba SC TP MAZEMBE WAWASILI SALAMA TANZANIA

TP MAZEMBE WAWASILI SALAMA TANZANIA

 KIKOSI cha TP Mazembe kutoka Congo tayari kimewasili ndani ya ardhi ya Bongo kwa ajili ya kushiriki Simba Super Cup.

TP Mazembe ni miongoni mwa timu tatu ambazo zitashiriki mashindano ya Simba Super Cup ambayo yanaanza kufanyika Leo Januari 27, Uwanja wa Mkapa. 

Timu nyingine ambazo zinashiriki ni pamoja na Al Hilal ya Sudan ambayo itaanza kucheza leo Januari 27 na wenyeji Simba, Uwanja wa Mkapa.

TP Mazembe itamenyana na Al Hilal Januari 29 na itakutana na Simba Januari 31 na mechi zote zitachezwa saa 11:00 jioni.

SOMA NA HII  WAKATI BOCCO AKILAUMIWA KWA KUKOSA MAGOLI...MBRAZILI SIMBA AFICHUA KILICHOWAPONZA..