ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amesema kuwa anavutiwa na viwango vya ubora wa nyota wa Simba huku akitabiri kuwa klabu hiyo msimu huu itafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Zahera ametoa kauli hiyo wakati ambapo Simba inajiandaa na michuano ya Simba Super Cup itakayoanza kutimua vumbi kesho na kushirikisha timu tatu ambazo ni; TP Mazembe ya DR Congo, Al Hilal ya Sudan na wenyeji Simba.
Michuano hiyo ni muhimu kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba imepangwa kundi A ikiwa na timu za Al Alhly ya Misri, As Vita ya DR Congo na Al Merrikh ya Sudani.
Akizungumzia ubora wa wachezaji wa Simba Zahera amesema: “Naamini Simba msimu huu itafika mbali katika ligi ya mabingwa kwa sababu wachezaji wengi wana uwezo wa michuano yenyewe.
“Lakini pia wamepata bahati ya kukutana na timu ambazo walishacheza nazo katika hatua hiyo misimu miwili iliyopita hivyo, ni suala la wao wenyewe kujipanga vizuri.
“Angalia mtu kama Chama, Kagere au Bocco (John), wote wamesheza msimu mmoja uliopita na walifanya vizuri sasa unadhani safari hii nini kitatokea na ikizingatiwa wamesajili wachezaji.
“Halafu kuna michuano ya Simba Super Cup ambayo ni wazi itawasaidia sana, naamini wanaweza kushangaza Afrika,”