Yanga SC

YANGA YAJIVUNIA KOMBE LA MAPINDUZI, KUONGOZA LIGI

admin February 4, 2021 10:47 am

 


UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema unajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata msimu huu kwa kutwaa taji la kombe la Mapinduzi, pamoja na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa.

Yanga mpaka sasa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi, ambapo wamejikusanyia pointi 44 baada ya kucheza michezo 18,  wakishinda mechi 13 na kutoa sare michezo mitano pekee.

Akizungumzia mipango na mafanikio yao msimu huu Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM na mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, Injinia, Hersi Said amesema: “Tumefanya uwekezaji mkubwa ndani ya kikosi chetu msimu huu, na sisi sote tunakubaliana kwamba tayari matunda yameanza kuonekana kupitia ubingwa wa mapinduzi na mwenendo mzuri kwenye ligi.

“Tunashukuru Mungu katika hilo na wakati huu tumebaki na lengo moja tu la kuhakikisha tunaibuka mabingwa msimu huu.

MITAMBO HII YA MABAO NI MWENDO WA NNENNE KOCHA AIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI AFRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply